Wednesday, 10 September 2014

Wizkid kuachia album mpya aliyowashirikisha Tyga, Akon na Wale

Star wa Nigeria, Wizkid ameshare cover ya album yake mpya anayotarajia kuiachia. Album hiyo ameiita jina lale halisi ‘Ayo’ ikimaanisha furaha (Joy). Jina kamili la mwimbaji huyo wa ‘Show You The Money’ ni Ayodeji Ibrahim Balogun

Katika album hiyo yenye nyimbo 18 na wimbo mmoja wa ziada (bonus), amewashirikisha wasanii mbalimbali wa Nigeria pamoja na wa kimataifa. Wasanii aliowashirikisha ni rapper wa YMCMB, Tyga, Akon, Femi Kuti, Seyi Shay, Phyno, Banky W na Wale.
Hii ni album ya pili kwa msanii huyo mwenye miaka 24, baada ya ile ya kwanza ‘Superstar’ iliyotoka 2011.

No comments:

Post a Comment