Friday, 5 June 2015

RAFAEL BENITEZ ASAINI MIAKA 3 REAL MADRID


Rafal Benitez atambulishwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Real Madrid leo. Asaini mkataba wa miaka mitatu.
 Aliyekuwa Kocha wa Napoli Rafa benitez amethibitishwa kuwa kocha wa Real madrid katika kandarasi ya miaka mitatu.

Benitez mwenye umri wa miaka 55anachukua mahala pake Carlo Anceloti ambaye aliondoka katika kalbu hiyo miezi 12 tu baada ya kusaidia kushinda kombe lao la kumi la vilabu binga ulaya.

Benitez ambaye ni mzaliwa wa Madrid amehudumu misimu miwili kama mkufunzi wa napoli baada ya kufanikiwa na vilabu kadhaa vya ulaya

Baada ya kusaidia Valencia kushinda kombe la Uefa 2004, mwaka unaofuatia alielekea Liverpool na kuisaidia kilabu hiyo kushinda kombe la vilabu bingwa ikiwa ni msimu wake wa kwanza katika kilabu hiyo ya Mersyside.

Miaka miwili aliisaidia kufika katika fainali za kombela vilabu bingwa ulaya na mwaka 2013 alikuwa kaimu mkufunzi wa chelsea waliposhinda kombe la Europa.



No comments:

Post a Comment