Saturday, 22 November 2014

ALLY KIBA AFUNGUKA MADAI YA KUTOMTUMIA R KELLY KAMA FURSA KWENYE MUZIKI WAKE

Mkali wa ngoma ya Mwana DSM, Ally Kiba kama unakumbuka alishiriki kwenye project ya One 8, ambayo baadhi ya wasanii wakubwa barani Afrika waliteuliwa na kwenda nchini Marekani wakakaa studio moja na msanii wa kimataifa R Kelly, ambaye aliwaandikia ngoma ya Hands Across The World na Wakai Record.



Ndani ya ngoma hiyo kuna sauti za wasanii kama 2face, Ali Kiba, Amani, Navio, JK, Movaizhaleine, Fally Ipupa. Project hiyo ilisimamiwa na Rock Star 4000, na Sony Music.
Sasa zengwe limeibuka hivi karibuni watu wakidai eti ally kiba hakuitumia nafasi hiyo kama fursa ya kuukuza muziki wake duniani nzima. Alikiba alisema kuwa zamani zile mitandao ya kijamii haikuwa kama sasa ndiyo maana halikusikika likapita lakini kati ya wasanii wote waliokuwepo kwenye project hiyo hawakufanya ngoma yoyote na R.Kelly,pia,pia muda ulichangia kila mtu alikuwa bize na shughuli zake.

No comments:

Post a Comment