Tuesday, 6 May 2014

Seneta wa Nairobi Mike Sonko ‘sharobaro’ ameamua kuonyesha mshahara anaolipwa na matumizi yake.


Unaambiwa Seneta wa Nairobi Mike Sonko maarufu kama mbunge Sharobaro time hizo, amepost payslip yake kwenye Facebook ikionyesha mshahara anaochukua na matumizi yake kwa mwezi March.

Mike Sonko anakua kiongozi wa kwanza nchini Kenya kuweka wazi kiasi cha pesa anachopokea kama mshahara na matumizi yake ambapo kwa mujibu wa jarida la NN au Nairobi News Payslip hiyo inaonyesha seneta Sonko anapokea mshahara wa shilingi 532,705 pesa za Kenya kila mwezi.

Seneta Sonko anadai kwamba pesa anayopokea hupeleka kanisani kama sadaka na mchango wake wakati wa hafla ya michango au Harambee.

Miongoni mwa matozo katika mshahara wake ni ya kulipa mkopo aliouchukua kutoka kwa benki ilikuwasaidia waathirika wa mkasa wa moto wa Sinai [mwaka wa 2011 alipokua mbunge wa Makadara] kufanyiwa upasuaji na kukimu ada ya hospitali.


Hii ndio list ya makanisa yanayopata pesa kutoka kwenye mshahara wa Sonko mwezi machi 2014.
Nairobi calvary temple Buruburu Ksh 50,000
Pentecostal church eastleigh (kiambio) Ksh 50,000
AIC Jericho Ksh 100,000
PCEA bahati Ksh 100,000
PCEA Kangemi Ksh 30,000
FPFK Church Kibera Ksh 30,000
Kawangware Methodist Ksh 30,000
PCEA Lunga Lunga Ksh 30,000
St. Francis Assis Mombasa Ksh 30,000
Sister Vivenzia memorial foundation Ksh 50,000
PCEA Umoja Ksh 30,000
PCEA Kangemi Ksh 30,000
Jesus winners ministry Roysambu Ksh 30,000
Makongeni SDA Kshs 40,000
St. Joseph Catholic Church Mumbi Muranga Ksh 200,000
AIC Yakamete Ngelani Ksh 100,000
Free Medical Camp in Deep Sea Slum Ksh 450,000
Teen Challenge Kenya rehab center Ksh 200,000

No comments:

Post a Comment