Liverpool wakiwa ugenini leo wameweza kushinda kwa magoli 3-2 dhidi ya Norwich.
Alikuwa Raheem Sterling aliyeanza kufungua akaunti ya magoli ya Liverpool leo katika dakika ya nne tu ya mchezo, Luis Suarez akaja kuongeza bao la dakika ya 11.
Baaada ya magoli hayo Norwich wakaja juu na kufanikiwa kupata goli kupitia Gary Hooper kwenye dakika ya 54 ya mchezo, ili kujihakikishia ushindi Sterling tena kwenye dakika ya 62 akaifungia Liverpool goli la tatu. Dakika 15 baadae Robert Snodgrass akafunga goli la pili upande wa Norwich.
No comments:
Post a Comment